Saturday, September 4, 2010

064

Kilicho na mizizi ni rahisi kupata lishe bora.
Kilicho bado kipya ni rahisi kusahihisha.
Kilicho kigumu ni rahisi kuvunjika.
Kilicho kidogo ni rahisi kukitawanya.

Zuia rabsha kabla haijaanza.
Panga vitu uzuri kabla havijakuwepo.
Mti mkubwa wa msonabari huanza kama mchicha dhaifu.
Safari ya maili elfu moja huanza chini ya miguu yako.

Kukimbilia kuanza kufanya jambo huishia kushindwa.
UKijaribu kuvikamata vitu huishia kuvipoteza.
UKikimbilia kukamilisha mradi huishia kuharibu kilichokuwa kimekwiva tayari.

Kwa hiyo gwiji hutekeleza mambo kwa kuachia yafuate mkondo wake yenyewe.
Huwa mtulivu yanapofikia mwisho kama alivyokuwa wakati yakianza.
Hana chochote, kwa hiyo hana lolote la kupoteza.
Alicho na ashiki nacho ni kukosa ashiki.
Anachojifunza ni kufuta alichokwishajifunza.
Huwa anawakumbusha watu kile tu ambacho tayari walishakuwa sikuzote.
Hana kingine anachokijali ila Tao tu.
Kwa hiyo anaweza kuvijali na kuviangalia vitu vyote.

AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]


Copyright © Sammy Makilla-2010

No comments:

Post a Comment