Ukamilifu wa kweli huonekana una mapungufu,
hali ya kuwa ndio ukamilifu wenyewe.
Kujaa kikweli kweli huonekana kitu kitupu,
hali ya kuwa kimejaa mpaka juu.
Kilichoonyoka hasa, huonekana kupinda.
Busara ya kweli huonekana ujinga.
Na sanaa ya kweli huonekana takataka.
Mwalimu huachia vitu vitokee vyenyewe.
Huumba matukio kwa jinsi yanavyotokea.
Hujiweka pembeni na kuiachia Tao kujizungumza yenyewe.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, September 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment