Ikiwa unataka kuwa kiongozi bora,
Lazima ujifunze kwanza kuifuata Tao.
Acha kutaka kudhibiti.
Achana na mipango isiyobadilika na dhana tasa,
Na dunia yako itaanza kujitawala yenyewe.
Kadri ulivyo na vikwazo na vizuizi vingi,
Ndivyo utakavyokuwa na watu wengi wasio waadilifu.
Kadri utakavyokuwa na silaha nyingi,
Ndivyo watu watakavyozidi kujiona sio salama.
Kadri unavyotoa ruzuku nyingi,
Ndivyo wananchi wanavyokuwa wategemezi zaidi.
Kwa hiyo gwiji hubainisha:
Huwa ninaachana na sheria,
Na ndivyo watu wanavyokuwa waaminifu zaidi.
Huwa ninaachana na uchumi,
na ndivyo watu wanavyofanikiwa kiuchumi zaidi.
Huwa ninaachana na dini,
Na ndivyo watu wanavyokuwa watulivu zaidi.
Huwa ninaachana na matamanio yote kwa manufaa ya walio wengi,
Na manufaa haya husambaa kila mahala kama majani.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, September 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment