Hapo mwanzo kulikuwa na Tao
Vitu vyote hutoka na kisha kurudi tena kwenye Tao.
Ili kujua asili ya kitu fuatilizia kwanza kuwepo kwake.
Unapowatambua watoto na kumuona mama yao,
huo utakuwa ni mwisho wa huzuni yako.
Ukiwa unawahukumu wengine duniani,
Na ukaanza kucheza na matamanio moyo wako utaanza kusumbuka.
Ikiwa hauwahukumu wengine na haauongozwi na matamanio yako basi moyo wako utakuwa katika amani.
Kuona katika giza ni ubayana.
Na kujua wakati wa kujisalimisha ni nguvu na uwezo.
Tumia mwanga wako mwenyewe ili urudi kwenye chanzo cha mwanga.
Hili linaitwa ni kufanya mazoezi ya utu wa milele.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, September 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment