Lililo jema na bora kabisa duniani ni kama maji,
yanayolisha watu wote bila ya kujaribu kufanya hivyo.
Huwa inaridhika na sehemu za chini ambako watu huwa hawapendi,
Kwa hiyo ni kama Tao.
Katika makazi ishi karibu kabisa na ardhi;
Katika kufikiri, fikiria kilicho chepesi na rahisi kabisa;
Katika ugomvi tenda haki na kuwa mkarimu.
Katika kutawala usijaribu kudhibiti.
Katika masuala ya kazi, fanya kazi uipendayo.
Na katika masuala ya familia, jaribu kuwepo saa zote kwa marefu na mapana yote.
Unapotosheka na kuwa kile uicho,
Na wala haujilinganishi wala kushindana na mtu,
kila binadamu atakuheshimu !
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Tuesday, September 7, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment