Mwalimu hana akili yake mwenyewe,
huwa anafanya kazi na akili za watu wengine.
Ni mwema kwa watu waliokuwa wema.
Ni mzuri pia kwa watu wasiokuwa wema.
Huu ndio wema wa kweli.
Huwaamini watu wanaoaminika.
Aidha, huwaamini pia watu wasioaminika.
Huu ni uaminifu wa kweli.
Akili ya Mwalimu ni kama anga za juu.
Hakuna anayemwelewa.
Humuangalia na kusubiri.
Naye huwachukulia watu kama watoto wake.
AYA ZA MTAWA
[ Tao-Te-Ching ]
Copyright © Sammy Makilla-2010
Sunday, September 5, 2010
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment